Dira

Kutoa ushawishi chanya katika maisha ya wengi kupitia Uvumbuzi na Ubunifu.

Dhamira

Kuunda utajiri na fursa za ajira katika Afrika pamoja na kuzidisha ukuaji wa kijamii na kiuchumi kwaajili ya wadau wetu.

Maadili ya Msingi

  • Ubunifu na Uvumbuzi
  • Uwajibikaji
  • Uwazi

Sisi ni nani

Transformation Hub Investment Group (THIG) ni kampuni iliyojikita kwenye uvumbuzi rahisi na yenye uchu wa maboresho ya vipato vya mamilioni ya watu wasio na fursa, wanaoishi katika jamii za nchi zinazoendelea kote barani Africa.

Kupitia miradi yetu ya kijamii (Turning Point , i-Hub na Sarafu), tunayalea maendeleo ya kudumu kwa kusudi la kupunguza umaskini, njaa na kutowiana kwa vipato katika nchi za Afrika zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara.

Timu yetu

THIG inaendeshwa na timu ya watu wabunifu na wenye ari ya hali ya juu walio na lengo moja la kuunda ukuaji maduhubuti, endelevu na wenye kuonekana kote barani Afrika. Hapa THIG, kila siku ni fursa ya kuvumbua na kutekeleza utatuzi uliotokea Afrika kwaajili ya Afrika.

Tukiwa watu waliokulia kwenye jamii zinazokabiliwa na changamoto kama hizo, tulivuviwa kuunda THIG ili kusaidia mamilioni ya wengine wanaokabiliana na mapambano haya leo. Kupitia kwetu mambo haya, uchu na unyumbukaji wetu vikifuatana na ujuzi wetu wa TEHAMA, Usimamizi wa Miradi, Kilimo na Shughuli za Kibenki vinaendelea kutuwezesha kupata mafanikio makuu katika kubadili jamii tunamoendesha shughuli zetu.

Msaada? Ongea Nasi