Tunafanya nini na taarifa zako?

Kama sehemu ya usajili, unapojiunga na huduma za majukwaa yetu ya mtandaoni, tunakusanya taarifa zako binafsi unazotupatia kama vile jina lako, anuani, barua pepe na namba ya simu.

Pia, pale unapotembelea jukwaa zetu mtandaoni, tunapokea anuani ya itifaki ya mtandao ya kompyuta yako (IP address) inayotusaidia kuufahamu mfumo wake.

Matangazo ya bidhaa kupitia barua pepe, SMS (kama imeruhusiwa): Tunaweza kukutumia barua pepe au ujumbe fupi (SMS) kuhusu huduma zetu, bidhaa mpya na dodoso nyingine.

Ridhaa

Mnapataje ridhaa yangu? Unapotupatia taarifa zako binafsi ili kuhitimisha muamala, kuhakiki kadi yako ya benki, kununua huduma, kupokea au kurudisha bidhaa, tunamaanisha umeridhia sisi kuzikusanya na kuzitumia kwaajili ya sababu hiyo tu.

Kama tukitaka taarifa zako kwaajili ya sababu nyingine kama vile kunadi bidhaa zetu zilizoko sokoni, tutakuomba moja kwa moja ili upate fursa ya kukubali au kukataa.

Nawezaje kukanusha ridhaa yangu? Kama baada ya kuingia ukabadili mawazo, unaruhusiwa wakati wowote kutukatalia; kuwasiliana na wewe, kuendelea kukusanya, kutumia au weka wazi taarifa zako kwa kuwasiliana nasi kupitia info@thigafrica.com au kwa barua kwenda Transformation Hub Investment Group, Kampala, Uganda.

Ufunuzi

Tunaweza weka wazi taarifa zako kama itatulazimu kisheria au kama utavunja masharti yetu ya huduma.

Majukwaa ya THIG

Majukwaa yetu yanashirikiwa na watoa huduma mbalimbali. Wanatupatia fursa ya kuwa na jukwaa la matandaoni la uchumi na michango ya watu wengi (crowdfunding) linalotuwezesha kukusanya fedha, kuuza bidhaa na huduma zetu kwako.

Taarifa zako zinahifadhiwa kwa njia ya hifadhi ya data ya THIG na programu ya jumla ya THIG Wanatunza taarifa zako kwenye seva salama na yenye ulinzi.

Malipo: Ukichagua malipo ya moja kwa moja kwenye kuhitimisha manunuzi yako, hapo THIG inatunza namba ya kadi yako ya benki au aina yoyote ya malipo utakayotumia na kuilinda kwa mfumo wa kanuni wa kompyuta. Taarifa za muamala wa manunuzi zitatunzwa tu kwa ule muda utakaouhitaji kuhitimisha muamala huo. Baada ya hapo, taarifa hizo hufutwa.

Kwa maelezo zaidi, soma Masharti ya Huduma ya THIG hapa au Maelezo Juu ya Sera ya Faragha hapa.

Watoa huduma binafsi tunaowatumia watakusanya

Kiujumla, watoa huduma binafsi tunaowatumia watakusanya, tumia na kutoa taarifa zako kwa ule umbali unaohitajika tu ili waweze kutupatia huduma tunazohitaji.

Hata hivyo, watoa huduma binafsi kadhaa, kama mikondo ya malipo na wachanganuzi wengine wa miamala ya malipo wana sera zao wenyewe za usalama juu ya taarifa tunazotakiwa kuwapa kwa ajili ya miamala yako ya manunuzi.

Kwa watoa huduma hawa, tunashauri kwamba usome sera zao za usalama ili uweze kuelewa jinsi watakavyo zisimamia taarifa zako.

Kumbuka pia baadhi ya watoa huduma wanaweza kuwapo au kuwa na nyenzo zilizopo chini ya mamlaka tofauti nawe au nasi. Hivyo, ukichagua kuendelea na muamala ambao unajumuisha huduma toka kwa watoa huduma binafsi, ndipo taarifa zako zinaweza kukwa chini ya sheria za mamlaka hiyo/hizo ambamo mtoa huduma huyo au nyenzo zake zinapatikana.

Kama mfano, kama upo Kanada na muamala wako unashughulikiwa na mikondo ya malipo iliyoko Marekani, taarifa zako zinazotumika kuhitimisha muamala huo zinaweza kutolewa/kusomwa kulingana na sheria za Marekani, hasa sheria yao ya uzalendo (Patriot Act).

Mara utokapo kwenye jukwaa zetu mtandaoni au umepelekwa kwenye tovuti au app ya mtoa huduma binafsi, hautakua tena chini ya Sera hii au Masharti ya Huduma zetu mtandaoni.

Viungo (Linki) Unapobofya linki kwenye majukwaa yetu, zinaweza kukupeleka nje ya tovuti zetu. Hatuhusiki na sera za usalama za tovuti nyinginezo na tunakusisitizia usome maelezo yao ya faragha.

Usalama

Kulinda taarifa zako binafsi, tunachukua tahadhari na kufuata mwenendo bora wa sekta hiyo kuhakikisha hazipotei, hazitumiki, hazifichuliwi, hazibadilishwi au kuharibiwa kizembe.

Ukitupatia taarifa zako za kadi ya benki, taarifa hii itafichwa kutumia teknolojia salama ya socket layer (SSL) na kutunzwa na uficho wa AES-256. Ingawa hakuna njia yoyote iliyo salama 100% ya utumaji au utunzaji data mtandaoni, tutafuata vigezo vyote vya PCI-DSS na kuweka viwango vya ziada vinavyokubalika kwenye sekta hiyo.

Umri wa kutoa ridhaa

Kwa kutumia majukwaa yetu ya mtandaoni, unaonesha kuwa una angalau umri wa utu uzima wa nchi au jimbo lako la makazi na umetoa ridhaa yako kuruhusu yoyote ya wategemezi wako wadogo/wenye umri mdogo kutumia tovuti hii.

Mabadiliko kwa hii Sera ya Faragha

Tunayo haki ya kurekebisha sera hii muda wowote, hivyo ipitie mara kwa mara. Mabadiliko na fafanuzi zitaanza kutumika mara moja baada ya kuwekwa kwenye majukwaa yetu mtandaoni. Kama tutafanya mabadiliko ya maudhui kwa sera hii, tutakuarifu hapa kwamba imesasishwa, ili uweze kufahamu ni taarifa gani tunakusanya, tunazitumiaje na ni katika hali gani tunazitumia na/au kuzitoa.

Kama kampuni itanunuliwa au kuungana na kampuni nyingine, taarifa zako zinaweza kuhamishwa kwa wamiliki wapya ili tuweze kuendelea kukuuzia bidhaa.

Maswali na mawasiliano

Kama utapenda: kupata, sahihisha, rekebisha au kufuta taarifa binafsi zozote tulizo nazo kukuhusu, kutoa lalamiko au kutaka tu maelezo zaidi wasiliana na Afisa Muandamizi Usalama kupitia info@thigafrica.com au kwa barua ya posta kupitia Transformation Hub Investment Group.
[Yah: Afisa Usalama Muandamizi] Kampala, Uganda.]

Msaada? Ongea Nasi