Maelezo jumla

Jukwaa hili la mtandaoni linaendeshwa na Transformation Hub Investment Group. Kila mahali kwenye jukwaa hili palipo na maneno au neno “sisi”, “nasi” , “yetu”, “wetu”, “vyetu” na “zetu” mara zote humaananisha Transformation Hub Investment Group. Transformation Hub Investment Group inatoa jukwaa hili, pamoja na taarifa, zana na huduma zote zinazopatikana humu kwako, wewe mtumiaji, pale utakapokubaliana na masharti, vigezo sera na ilani zote zilizoelezewa hapa.

Kwa kutembelea majukwaa yetu na/au kununua huduma kutoka kwetu, unashiriki “huduma” yetu na unakubali kufungwa na vigezo na masharti vifuatavyo (“Masharti ya Huduma”, “Masharti”), yakiwemo masharti na vigezo na sera za ziada zinazoelezwa humu na/au kupatikana kwa kiungo-hipa. Masharti haya ni kwa watumiaji wote wa majukwaa yetu, wakiwemo watumiaji ambao ni wasomaji, wachuuzi, wateja, wafanyabiashara na/au wachangiaji maudhui.

Tafadhali soma Masharti ya Huduma kwa makini kabla ya kupata au kutumia majukwaa yetu. Kwa kuingia au kutumia sehemu yoyote ya jukwaa letu mtandaoni, unakubali kufungwa na haya Masharti ya Huduma. Kama hukubaliani na masharti na vigezo vyote vya makubaliano haya, ndipo hutoweza kutumia majukwa au huduma zetu zozote. Kama haya Masharti ya Huduma yatachukuliwa kama ofa, kukubalika kuko chini ya masharti hayo.

Pia, sehemu au nyenzo zozote mpya zitakazoongezwa kwenye majukwaa yaliyopo, zitakuwa chini ya Masharti ya Huduma. Unaweza kupitia toleo la karibuni zaidi la Masharti ya Huduma wakati wowote hapa. Tuna haki ya kusaihisha, kugeuza au kubadili sehemu yoyote ya haya Masharti ya Huduma kwa kutuma dodoso na/au mabadiliko kwenye majukwaa yetu ya mtandaoni. Ni wajibu wako kupitia ukurasa huu kila mara ili kujua kama kuna mabadiliko yoyote.

Kuendelea kwako kutumia majukwaa yetu ya mtandaoni baada ya kuwekwa mabadiliko yoyote yale inaashiria kukubaliana kwako na mabadiliko hayo. Jukwaa letu linabebwa na watoa huduma mbalimbali. Wanatupatia majukwaa ya biashara mtandao yanayotuwezesha kukuuzia bidhaa na huduma zetu.

Masharti ya jukwaa la mtandaoni

Kwa kukubaliana na haya Masharti ya Huduma, unasema kwamba una angalau umri wa utu uzima wa nchi au jimbo lako la makazi na umetoa ridhaa yako kuruhusu yoyote ya wategemezi wako wadogo/wenye umri mdogo kutumia tovuti hii.

Haupaswi kutumia bidhaa zetu kwa kusudi lolote haramu au lisiloidhinishwa wala haupaswi, katika matumizi ya huduma, kukiuka sheria zozote katika mamlaka yako (pamoja na lakini si kwa udogo sheria ya hakimiliki).

Haupaswi kutuma virusi au kanuni zozote za uharibifu za kompyuta.

Kuvunja au kukiuka hata moja ya masharti haya itapelekea kusimamishwa mara moja kwa huduma au matumizi yako.

Vigezo jumla

Tuna haki ya kukataa kutoa huduma kwa mtu yoyote kwa sababu yoyote kwa muda wowote.Unaelewa kwamba taarifa zako (ukiondoa taarifa za kadi ya benki), zinaweza kuhamishwa zikiwa hazijafichwa na kuhusisha (a) utumwaji kwenye mitandao mbalimbali; na (b) mabadiliko ya kuzingatia na ya kukabiliana na mahitaji ya kiufundi ya kuunganisha mitandao au vifaa. Taarifa za kadi za benki hufichwa mara zote wakati wa uhamisho mitandaoni. Unakubali kutozalisha, rudia, nakili, uza, uza tena au tumia sehemu yoyote ya huduma, matumizi ya huduma au upatikanaji wa huduma au mawasiliano yoyote kwenye majukwa kupitia huduma iliyotolewa, bila ya idhini ya maandishi kutoka kwetu. Dibaji zinazotumiwa kwenye makubaliano haya zimejumuishwa kwaajili ya kurahisisha tu na hazitapunja au kuathiri masharti haya.

Transformation Hub Investment Group, ikijiendesha kwa jina la biashara THIG ni kampuni binafsi (Limited) iliyosajiliwa katika mataifa kadhaa ya Afrika, hususani Mashariki mwa Afrika na hivi karibuni itapanua wigo wake katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Majukwaa ya THIG, bidhaa, nembo na chapa ni Hati miliki na Usajili wa Alama ya Biashara ya Shirika ya Transformation Hub Investment Group, uingizaji, uchapishaji wa majukwaa ya THIG na bidhaa zake hazikubaliki bila idhini yetu kwa maandishi.

Wadau wetu wanashauriwa sana kutafuta ushauri wa kitaalamu wa kujitegemea wakati wa kuzingatia kufanya uwekezaji na THIG. Kwa wawekezaji, tunakuhimiza kupata ushauri huru wa kisheria na kifedha kabla ya kufanya uwekezaji. Kwa wafadhili wetu, utimilifu, uwajibikaji na uwazi ni nguzo zetu muhimu, tunaahidi kutoa huduma zetu kwa kiwango cha juu cha utimilifu, uwajibikaji, na kuwa wazi katika shughuli zetu zote.

Usahihi, umtimilifu na muda sahihi wa taarifa

Hatuwajibiki kama taarifa zinazopatikana kwenye tovuti hii si sahihi, kamili au za wakati huo. Kilichomo kwenye tovuti hii kimetolewa kwaajili ya taarifa jumla tu na zisitegemewe au kutumiwa kama chanzo pekee cha kufanyia maamuzi bila ya ushauri msingi wa vyanzo sahihi, kamili na vya wakati zaidi vya taarifa. Kutegemea tu yaliyomo kwenye tovuti hii ni hatari kwako mwenyewe.

Tovuti hii inaweza kuwa na habari fulani za/ya kihistoria. Taarifa za kihistoria, hasa, si za wakati huo na zinatumiwa kwaajili ya kukurejeza tu. Tuna haki ya kurekebisha yaliyomo kwenye tovuti hii wakati wowote, lakini hatuna lazima ya kusaihisha taarifa yoyote kwenye tovuti yetu. Unakubali kuwa ni wajibu wako kufuatilia mabadiliko kwenye tovuti yetu.

Marekebisho ya huduma na bei

Bei za bidhaa zetu zinaweza kubadilika bila taarifa.

Tuna haki ya kuirekebisha au kukatisha Huduma (sehemu au yaliyomo yoyote) wakati wowote bila taarifa.

Hatuwajibiki kwako au kwa watoa huduma binafsi kwa marekebisho, badiliko la bei, kusimamishwa au kukatishwa kokote kwa huduma.

Bidhaa au huduma (kama inafaa)

Bidhaa au huduma kadhaa zinaweza kupatikana mtandaoni peke yake kupitia tovuti au programu za simu. Hizi huduma au bidhaa zinaweza kuwa na ubora mdogo na zinaweza kurudishwa au kubadilishwa kulingana na Sera yetu ya Marejesho tu.

Tumejitahidi sana kuonesha kwa sahihi iwezekanavyo rangi na picha za bidhaa zetu zinazoonekana kwenye majukwaa yetu. Hatuwezi kukukuhakikishia kwamba kompyuta yako itaonesha rangi kwa hizo katika usahihi.

Tuna haki ya, lakini hatulazimiki, kupunguza uuzaji wa bidhaa zetu au huduma kwa mtu, eneo la kijiografia au mamlaka yoyote. Tunaweza kutumia haki hii kulingana na kesi yenyewe. Tuna haki ya kupunguza idadi ya bidhaa au huduma zozote tunazotoa. Bidhaa zote au bei za bidhaa zinaweza kubadilika wakati wowote bila taarifa, pale tutakapoona vema. Tuna haki ya kuondoa bidhaa yoyote wakati wowote. Ofa kwa bidhaa au huduma yoyote itakayokuwa imezuiwa ni batili.

Hatuwezi kukukuhakikishia kuwa ubora wa bidhaa, huduma, habari, au vifaa vingine vyovyote ulivyonununua au kupata vitakidhi matarajio yako, au kwamba makosa yoyote katika Huduma yatarekebishwa.

Usahihi wa taarifa za malipo na akaunti

Tuna haki ya kukataa oda yoyote utakayotupa. Ikiwa inafaa, tunaweza kupunguza au kufuta idadi ya manunuzi kwa mtu, kwa kaya au kwa oda moja. Vizuizi hivi vinaweza kujumuisha oda zilizotolewa kupitia au kuwa chini ya akaunti ya mteja mmoja, kadi ya benk moja, na/au oda zinazotumia anuani moja ya malipo na/au usafirishaji. Kama kukiwa na kubadilika au kufutwa kwa oda, tunaweza jaribu kukujulisha kwa kuwasiliana na barua pepe na/au anuani ya malipo/namba ya simu iliyotolewa wakati wa kutuma oda. Tuna haki ya kupunguza au kuzuia oda ambazo zimeonekana kutumwa na wauzaji au wasambazaji.

Unakubali kutoa taarifa za sasa, kamili na sahihi za manunuzi na akaunti kwaajili ya manunuzi yatakayofanyika kwenye majukwaa haya. Unakubali kusaihisha mara moja akaunti yako na taarifa nyingine, ikiwa ni pamoja na barua pepe, kadi za benki na tarehe zao za kuisha, ili tuweze kutimiza miamala yako na kuwasiliana nawe pale inapohitajika.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali pitia Sera yetu ya marejesho.

Nyenzo Zingine

Tunaweza kukupatia nyenzo za mhusika wa tatu ambazo hatuwezi kufuatilia, kudhibiti wala kujazia.

Unatambua na kukubali kwamba tunakupa nyenzo hizi “kama zilivyo” na “kama zipatikanavyo” bila ya waranti zozote, taswira au hali za aina yoyote na bila mapendekezo yoyote. Hatuhusiki na lolote litakaloinuka au linalohusiana na maamuzi yako ya kutumia nyenzo hiari za mhusika wa tatu.

Matumizi yoyote ya nyenzo hiari zinazotolewa kupitia tovuti yetu ni kwa hatari na maoni yako mwenye na uhakikishe unayafahamu na kukubaliana na masharti ya wa/mtoa huduma wanao/anayetoa zana hizo.

Hapo baadae tunaweza kutoa huduma mpya na/au vipengele kupitia majukwaa yetu (ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa zana mpya). Vipengele kama hivyo vipya na/au huduma zitakuwa pia chini ya haya Masharti ya Huduma.

Linki za mhusika wa tatu

Maudhui, bidhaa na huduma fulani zinazopatikana kupitia huduma yetu vinaweza kujumuisha mambo kutoka kwa wahusika wa tatu.

Linki za mhusika wa tatu kwenye tovuti hii zinaweza kukupeleka kwenye tovuti ambazo hazishirikiani nasi. Hatuhusiki na kuchunguza au kutathmini maudhui au usahihi wake na hatuthibitishi wala hatuhusiki na hatuwajibiki na vitu, tovuti, zana, bidhaa, au huduma zingine zozote za mhusika wa tatu.

Hatuhusiki na madhara au uharibifu wowote unaohusiana na manunuzi au matumizi ya bidhaa, huduma, rasilimali, maudhui au miamala mingineyo itakayofanyika, inayohusisha tovuti za mhusika wa tatu.

Tafadhali pitia kwa makini sera na shughuli za mhusika wa tatu na uhakikishe unazielewa kabla ya kufanya muamala wowote. Malalamiko, madai, wasiwasi, au maswali kuhusiana na bidhaa za mhusika wa tatu yaelekezwe kwa mhusika huyo.

Maoni, majibu na mawasilisho mengineyo ya watumiaji

Ikiwa, kwa ombi letu utatuma maoni fulani maalum (kwa mfano kuingia kwenye shindano) au bila ya ombi letu ukatutumia mawazo ya kibunifu, mapendekezo, mipango au rasilimali nyingine, iwe mtandaoni, kwa barua pepe, barua ya posta, au vinginevyo (kwa ujumla ‘maoni’), unakubali kwamba muda wowote bila kizuizi tunaweza hariri, nakili, chapisha, tangaza, gawatafsiri na kutumia kwa vyovyote na kwa njia yoyote maoni yoyote utakayotutumia. Hatulazimika na hatutawajibika (1) kutunza usiri wa maoni yako; (2) kulipia fidia maoni yoyote; au (3) kujibu manoni yoyote.

Tunaweza, lakini hatulazimiki, kufuatilia, kuhariri au kuondoa maudhui ambayo tunaweza amua kwa mtazamo wetu kuwa ni kinyume cha sheria, ya kuudhi, kutishia, uongo, kuharibu, ponografia, matusi au yasiyokubalika kwa vyovyote au ya kukiuka mali akili ya mhusika yoyote au haya masharti ya huduma.

Unakubali kwamba maoni yako hayata kiuka haki yoyote ya mhusika wa tatu, ikiwa ni pamoja na hakimiliki, alama ya biashara, faragha, utu au haki yote binafsi au ya umiliki. Unakubali zaidi kwamba maoni yako hayatakuwa na uongo au kuwa kinyume cha sheria, yakuumiza au machafuzi, au kuwa na kirusi chochote cha kompyuta au programu nyinge haribifu amabazo zinaweza kuathiri uendeshaji huduma au majukwaa yoyote husika ya mtandaoni. Hupaswi kutumia barua pepe bandia, kujifanya kuwa mtu mwingine, au kwa vyovyote vile kutupotosha sisi au wahusika wa tatu juu ya chanzo cha maoni yako.

Unawajibika binafsi na maoni yoyote utakayotoa na usahihi wake. Hatuwajibiki na hatuhusiki na maoni yoyote yanayowekwa humu nawe au mhusika wa tatu.

Taarifa binafsi

Kuwasilisha kwako taarifa binafsi kupitia majukwaa yetu kunaongozwa na Sera yetu ya Faragha. Kuona zaidi soma Sera ya Faragha

Makosa, ukosefu wa umakini na mapungufu

Mara kadhaa kunaweza kukawapo na taarifa kwenye majukwaa yetu au kwenye huduma zilizo na makosa ya uchapaji, usahihi, au kuachwa/kuondolewa kwa taarifa ambayo yanaweza kuhusiana na maelezo ya bidhaa, bei, promosheni, ofa, gharama za usafirishaji bidhaa, mida ya usafiri na upatikanaji. Tunayo haki ya kurekebisha makosa, kukosa umakini/usahihi au kuachwa/kuondolewa kwa taarifa, na kubadili au kusaihisha taarifa au kufuta oda kama taarifa kwenye huduma au majukwaa yoyote husika si sahihi wakati wowote bila ya taarifa (hata baada ya kuwasilisha oda yako).

Hatulazimiki kusaihisha, rekebisha au fafanua taarifa kwenye huduma au majukwaa yoyote husika ya mtandaoni, ikiwa ni pamoja na bila kizuizi, taarifa za bei, isipokuwa ikitulazimu kisheria. Hakuna tarehe maalum au tarehe ya toleo jipya inayotumika kwenye Huduma au majukwaa yoyote inapaswa kuchukuliwa kama ndiyo kiashiria cha kuwa taarifa zote za kwenye huduma au majukwaa husika zimerekebishwa au kusasishwa.

Matumizi yaliyokatazwa

Pamoja na makatazo mengine yaliyowekwa kwenye Masharti ya Huduma, ni marufuku kutumia tovuti au maudhui yake (a) kwa kusudi lililo kinyume na sheria; (b) kuomba wengine wafanye au washiriki vitendo haramu; (c) kukiuka masharti, kanuni, sheria, misingi au desturi zozote za kimataifa, kitaifa, kijimbo au kimkoa; (d) kuvunja au kukiuka haki zetu au za wengine za mali-akili; (e) kusumbua, kunyanyasa, kutusi, kuumiza, kuchafua jina la mtu, kukashifu, kupuuza, kutishia au kubagua kulingana na jinsia, matakwa ya kimapenzi, dini, kabila, rangi, umri, utaifa, au ulemavu; (f) kuwasilisha taarifa za uongo au potofu; (g) kutuma virusi au programu yoyote haribifu ambayo itatumika na inaweza kutumika kwa njia yoyote ile kuathiri ufanisi au uendeshwaji wa huduma; (h) kukusanya au kufuatilia taarifa binafsi za wengine; (i) kujaza masanduku ya barua pepe za watu, kufanya unakili haramu mtandaoni, kusingizia, kupekua au kuparaza; (j) kuchafua, kutusi au kusudi lolote baya; au (k) kuingilia au kuzunguka vipengele vya usalama vya huduma au majukwaa, tovuti zozote au intaneti. Tunayo haki ya kusitisha matumizi yako ya huduma au majukwaa mengine ukikiuka matumizi yaliyokatazwa.

Makanushi ya udhamini; mipaka ya dhima

Hatutoi uhakika wala dhamana kuwa matumizi ya huduma yetu hayatakatishwa, wala kuchelewa, salama au yasiyo na makosa.

Hatukuhakikishii kwamba matokeo ambayo yanaweza kupatikana kupitia matumizi ya huduma yatakuwa sahihi au ya kuaminika.

Unakubali kwamba mara kwa mara tunaweza kuondoa huduma kwa vipindi virefu au kufuta huduma bila ya kutoa taarifa kwako.

Unakubali kabisa kwamba, kutumia ama kushindwa kutumia huduma ni juu yako mwenyewe. Huduma na bidhaa zote na huduma unazozipata kupitia huduma hii mbali na maelezo yetu), zinatolewa “kama zilivyo” na “kama zinavyopatikana” kwa matumizi bila ya kuoneshwa, dhamana au hali ya vigezo vyoyote, vilivyoelezwa au kudokezwa, ikiwa ni pamoja na waranti au vigezo vyovyote vya kibiashara, ubora unaouzika, uzima kwaajili ya kusudi fulani, ustahimilivu, jina, na kutopenyeka.

Transformation Hub Investment Group, wakurugenzi , maafisa, wafanyakazi, wahisani, mawakala, wakandarasi, wanagenzi, waletaji, watoa huduma au leseni, hawahusiki na jeraha, upotevu, madai, au hasara yoyote iliyo/isiyo ya moja kwa moja, ndogo, maalum, au yenye madhara yoyote, ikiwa ni pamoja na faida, mapato, akiba na data zilizopotea, gharama za badilisho au hasara kama hizo, ziwe zimetokana na mkataba, kuvunjwa kwa makubaliano/mkataba (ikiwa ni pamoja na uzembe), dhima yoyote itakayojitokeza sababu ya kutumia huduma au bidhaa yoyote iliyopatikana kwa kupitia huduma hii, au kwa madai yanayohusika kwa vyovyote na matumizi yako ya huduma au bidhaa yoyote, ikiwa ni pamoja na bila kuacha, makosa au kuachwa/kusahaulika katika maudhui yoyote au hasara ya aina yoyote iliyo matokeo ya kutumia huduma au mauduhui yoyote (au bidhaa) iliyowekwa, tumwa au kupatikana kupitia huduma hii, hata kama tukiambiwa kuihusu. Kwasababu nchi au mamlaka nyingine haziruhusu kujitoa kwenye uhusika wa dhima kwa hasara zenye madhara; kwa nchi au mamlaka hizo, uhusika wetu utaenda umbali tu unaotulazimu kisheria.

Malipo ya fidia

Unakubali kulipa fidia, kutetea na kuona hawana madhara Transformation Hub Investment Group na kampuni mama, kampuni tegemezi, wahisani, washirika, maafisa, wakurugenzi, mawakala, wakandarasi, watoa leseni na huduma, wakandarasi wadogo, waletaji, wanagenzi na wafanyakazi, kutoka kwa madai au matakwa yoyote, ikiwa ni pamoja na ada ya mwanasheria, yaliyofanywa na mhusika wa tatu yoyote baada au kutokana na kuvunjwa kwa haya Masharti ya Huduma au nyaraka wanazoingiza kwa kumbukumbu au kukiuka kwako sheria yoyote au haki za mhusika wa tatu.

Kusitisha

Katika tukio kwamba utoaji wowote wa haya Masharti ya Huduma utabainika kuwa kinyume cha sheria, tupu au hayatekelezeki, hata hivyo, utoaji utatekelezeka kwa uwezekano wa juu kabisa utakaoruhusiwa kisheria na sehemu isiyotekelezeka itachukuliwa kana kwamba imesitishwa kutoka kwenye Masharti ya Huduma, na maamuzi hayo hayataathiri uhalali na utekelezaji wa utoaji mwingine unakaosalia.

Kikomo

Wajibu na dhima kwa wahusika watakaokutwa nao kabla ya tarehe ya kikomo zitavuka kikomo cha makubaliano haya kwa makusudi yote.

Haya Masharti ya Huduma yanafaa tu isipokuwa na mpaka yamekomeshwa nasi au nawe. Unaweza kukomesha Masharti haya ya Huduma wakati wowote kwa kutujulisha kwamba huhitaji tena kutumia huduma zetu au unapoacha kutumia tovuti yetu. Tukigundua utashindwa, au tukahisi umeshindwa kufuata sharti lolote au utoaji wa Masharti ya Huduma, tutakomesha pia makubaliano haya muda wowote bila ya taarifa na utawajibika na kiasi chote kinachodaiwa mpaka cha tarehe ya kikomo; na/au kukukatalia kupata au kutumia huduma zetu (au sehemu yake).

Makubaliano mazima

Kushindwa kuzingatia au kutekeleza haki yoyote ya utoaji wa haya Masharti ya Huduma hakutajumuisha msamaha wa haki hiyo wala utoaji.

Masharti haya ya Huduma na sera nyinginezo zozote au kanuni za uendeshaji tunazoziweka kwenye majukwaa yetu au kwa kuzingatia hii Huduma, yanajumuisha makubaliano mazima na maelewano kati yako na sisi na kuongoza matumizi yako ya Huduma hii, ikivuka makubaliano mengine yoyote ya awali au ya wakati ule ule, mawasiliano na mapendekezo, yawe ya kinywa au maandishi kati yetu sisi na wewe (ikiwa ni pamoja na matoleo ya awali ya Masharti ya Huduma).

Utata wowote kwenye utafsiri wa Masharti haya ya Huduma hautachukuliwa dhidi ya mtafsiri.

Sheria tawala

Haya Masharti ya Huduma na makubaliano mengine tofauti ambayo tunatolea huduma yataongozwa na kuundwa kulingana na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Uganda au mamlaka nyingine yoyote tutakayo fanya kazi chini yake.

Taarifa za mawasiliano

Maswali kuhusu Masharti ya huduma yatumwe kwetu kupitia info@thigafrica.com

Mabadiliko ya Masharti ya Huduma

Unaweza kupitia toleo la hivi karibuni la Masharti ya Huduma muda wowote kwenye majukwaa yetu.

Tunayo haki ya kusaihisha, kubadili sehemu yoyote ya haya Masharti ya Huduma kwa kuweka dodoso na mabadiliko kwenye majukwaa yetu mtandaoni. Ni jukumu lako kuangalia majukwaa yetu mara kwa mara kwaajili ya mabadiliko hayo. Kwa kuendelea kutumia majukwaa yetu ya mtandaoni au huduma hii kufuatia kuwekwa kwa mabadiliko ya haya Masharti ya huduma inaonesha kukubali kwako mabadiliko hayo.

Msaada? Ongea Nasi